Usindikaji wa Dagaa na Samaki
Kozi ya Usindikaji wa Dagaa na Samaki imeandaliwa kuwapatia washiriki maarifa na ujuzi wa vitendo kuhusu mbinu bora za usindikaji, uhifadhi, ufungashaji na uongezaji thamani wa dagaa na samaki ili kuongeza ubora wa bidhaa, kupunguza upotevu baada ya mavuno na kuongeza fursa za masoko. Washiriki watajifunza kanuni za usalama wa chakula, usafi katika uzalishaji, matumizi sahihi ya vifaa vya usindikaji, pamoja na viwango vya ubora vinavyohitajika katika soko la ndani na nje ya nchi.